SUA Kampasi ya Mizengo Pinda Yachochea Ndoto za Wanafunzi Halmashauri ya Mpimbwe kupitia Ziara ya Hamasa.

Katika jitihada za kusogeza elimu ya juu karibu na jamii na kuibua hamasa ya kimasomo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), kupitia Kampasi yake ya Mizengo Pinda, kimehitimisha ziara maalum ya utoaji wa hamasa na elimu ya udahili katika shule kumi (10) za sekondari ndani ya Halmashauri ya Mpimbwe.

Ziara hiyo ililenga mahususi wanafunzi wa Kidato cha Nne na Kidato cha Sita, ikiwahimiza kuongeza juhudi katika masomo yao ili kukidhi vigezo vya kujiunga na elimu ya juu. Kampasi ya Mizengo Pinda imetumia fursa hiyo kuonyesha wigo mpana wa fursa za kimasomo zilizopo SUA, huku ikijikita katika kuwajengea wanafunzi uelewa wa kozi zinazoendana na rasilimali za mazingira yao.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Afisa Udahili wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Ndg. Abel Lugimba, amesisitiza kuwa chuo hicho kimejipanga kutoa elimu yenye tija (competence-based education) ambayo inamlenga mhitimu kuwa na uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa katika sekta za kimkakati.

Afisa Udahili wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Ndg. Abel Lugimba akizungumza na wanafunzi wakati wa ziara ya kutembelea shule za sekondari ndani ya Halmashauri ya Mpimbwe.

Ndg. Lugimba alibainisha kozi zinazotolewa kwa sasa katika Kampasi hiyo ni Shahada ya Sayansi katika Usimamizi wa Rasilimali Nyuki (BSc. Bee Resources Management), Stashahada ya Utalii na Uwindaji wa Wanyamapori (Diploma in Tourism and Wildlife Hunting), Stashahada ya Uzalishaji na Usimamizi wa Mazao (Diploma in Crop Production and Management), na Stashahada ya Usimamizi wa Rasilimali Nyuki (Diploma in Bee Resources Management).

Afisa Udahili wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Ndg. Abel Lugimba akizungumza na wanafunzi wakati wa ziara ya kutembelea shule za sekondari ndani ya Halmashauri ya Mpimbwe.

Katika kuitikia mabadiliko ya soko la ajira, Ndg. Lugimba alieleza kuwa chuo kinaendelea na maboresho makubwa ya mitaala. Maboresho haya yanalenga kuanzisha kozi mpya na bunifu hapo baadaye, jambo litakalotoa wigo mpana zaidi wa uchaguzi kwa wahitimu wa sekondari wanaotaka kujiunga na chuo hicho.

Afisa Udahili wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Ndg. Abel Lugimba akizungumza na wanafunzi wakati wa ziara ya kutembelea shule za sekondari ndani ya Halmashauri ya Mpimbwe.

kuunga mkono jitihada hizo za chuo, Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mizengo Pinda, ametoa ofa ya kipekee kwa kuahidi kuwafadhili vijana kumi (10) wanaotoka katika Halmashauri ya Mpimbwe kwa kuwalipia ada ya masomo. Ahadi hiyo imetolewa kama sehemu ya kuwahamasisha wazazi na walezi wa eneo hilo kuwapeleka vijana wao kujiunga na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Kampasi ya Mizengo Pinda, ili kupata ujuzi utakaosaidia kuleta mapinduzi ya kiuchumi katika familia zao na jamii kwa ujumla.

Akiitimisha ziara hiyo, Afisa Udaili huyo ametoa rai kwa wanafunzi, walimu, na wakazi wa Halmashauri ya Mpimbwe na Mkoa wa Katavi kwa ujumla, kukichukulia Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) Kampasi ya Mizengo Pinda kama kitovu cha maarifa na ukombozi wa kifikra. Amewataka wadau hao kukitumia chuo katika nyanja za utafiti na ushauri wa kitaalamu ili kuchochea maendeleo ya elimu na uchumi katika kanda hiyo.

 

Related Posts

Mwenyekiti wa Bodi, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Kampasi ya Mizengo Pinda, Dkt. Zacharia Malley aongoza shughuli ya upandaji miti SUA Kampasi ya Mizengo Pinda

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Kampasi ya Mizengo Pinda, Dkt. Zacharia Malley, ameongoza shughuli...

Final Year Bee Resources Management Students of SUA Mizengo Pinda Campus Defend Special Projects

On February 19, 2026, thirty-eight final year students pursuing a Bachelor of Science in Bee Resources Management at the Mizengo...

Prof. Anna Sikira Urges First-Year Students at Mizengo Pinda Campus to Become Ethical Leaders and Responsible Citizens

Mizengo Pinda Campus, Sokoine University of Agriculture—21 November 2025 Sokoine University of Agriculture (SUA), Mizengo Pinda Campus, has concluded a...

Leave a Reply