SUA KAMPASI YA MIZENGO PINDA YAZITIKISA SHULE ZA SEKONDARI MLELE: YAHAMASISHA TAALUMA NA KUTANGAZA FURSA ZA UDAHILI

Katika juhudi za kuendeleza hamasa ya kielimu na kusogeza huduma za elimu ya juu karibu na jamii, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Kampasi ya Mizengo Pinda, kimefanya ziara maalum katika shule za sekondari zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Lengo kuu la ziara hiyo limeelezwa kuwa ni kuwajengea wanafunzi morali ya kusoma kwa bidii ili kufikia vigezo vya kujiunga na masomo ya juu, huku wakitambua fursa mbalimbali za kimasomo zinazotolewa na kampasi hiyo iliyopo jirani nao.

Akizungumza na wanafunzi kwa nyakati tofauti wakati wa ziara hiyo, Afisa Udahili wa Kampasi ya Mizengo Pinda, Ndg. Abel Lugimba, amewataka wanafunzi wa sekondari kuacha kubweteka na badala yake waongeze juhudi kwenye masomo yao ili wapate alama zitakazowafungulia milango ya kujiunga na Chuo Kikuu.

“Lengo letu ni kuona vijana wa Mlele na maeneo jirani wanatumia fursa ya kuwepo kwa Kampasi hii ya Mizengo Pinda hapa mkoani Katavi. Ili ufike hapa, ni lazima usome kwa bidii sasa. Chuo kipo tayari kuwapokea, lakini funguo ya kuingilia ipo mikononi mwenu kupitia matokeo mazuri ya mitihani yenu,” alisema Ndg. Lugimba.

Mbali na hamasa hiyo ya kitaaluma, Ndg. Lugimba alitumia fursa hiyo kutangaza na kufafanua kozi mbalimbali zinazotolewa na SUA katika kampasi hiyo, akisisitiza kuwa mitaala yao imelenga kuzalisha wataalamu watakaokabiliana na changamoto za soko la ajira na kujiajiri, hususan katika sekta za kilimo, mifugo, na usimamizi wa rasilimali.

 

Ziara hiyo imepokelewa kwa mikono miwili na walimu pamoja na wanafunzi wa shule hizo, ambao wamekiri kuwa uwepo wa maafisa kutoka SUA umewafungua macho kuhusu vigezo vya kujiunga na chuo kikuu na kuwapa picha halisi ya maisha ya kutaaluma yanayowasubiri.

Kampasi ya Mizengo Pinda inaendelea kuwa kitovu muhimu cha elimu mkoani Katavi, ikiwa na azma ya kubadilisha maisha ya jamii kupitia mafunzo, utafiti, na ushauri wa kitaalamu.

Related Posts

SUA Kampasi ya Mizengo Pinda Yachochea Ndoto za Wanafunzi Halmashauri ya Mpimbwe kupitia Ziara ya Hamasa.

Katika jitihada za kusogeza elimu ya juu karibu na jamii na kuibua hamasa ya kimasomo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha...

Mwenyekiti wa Bodi, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Kampasi ya Mizengo Pinda, Dkt. Zacharia Malley aongoza shughuli ya upandaji miti SUA Kampasi ya Mizengo Pinda

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Kampasi ya Mizengo Pinda, Dkt. Zacharia Malley, ameongoza shughuli...

Final Year Bee Resources Management Students of SUA Mizengo Pinda Campus Defend Special Projects

On February 19, 2026, thirty-eight final year students pursuing a Bachelor of Science in Bee Resources Management at the Mizengo...

Leave a Reply