Wafanyakazi na Wawakilisji wa Wanafunzi wa Kampasi ya Mizengo Pinda Wapatiwa Elimu ya Masuala ya Kijinsia Na Wataalamu Wabobevu Kutoka Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo

Prof John Jeckoniah, Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia kwenye Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) akiwasilisha mada ya masuala ya kijinsia kwa wafanyakazi na wawakilishi wa wanafunzi wa Kampasi ya Mizengo Pinda

Mtaalamu wa masuala ya Jinsia kwenye Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) Prof John Jeckoniah amesema kuwa malengo ya mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wafanyakazi na wanafunzi juu ya masuala ya Jinsia katika maeneo yao ili kuondoa unyanyasaji na ukatili wa masuala ya kijinsia pamoja na ukatili wa kingono.

Prof Jeckoniah amesema  kuwa kupitia mafunzo hayo na Uanzishwaji wa Kitengo na Dawati la Jinsia katika Chuo litasaidia kuondoa changamoto na matukio ya Unyanyasaji  wa Kijinsia na kingono na matukio yaliyokuwa yakiripotiwa mara kwa mara kwenye Vyuo mbalimbali na Taasisi nyingine.

Pia Prof Jeckoniah amesema Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Tayari kimeandaa sera ya masuala ya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia na muongozo wa uanzishwaji wa kitengo cha Jinsia na Dawati la Jinsia.

Mwisho Prof Jeckoniah Amewataka washiriki wa mafunzo hayo kutumia vyema Elimu hiyo ili kusaidia Jamii kuondokana na Unyanyasaji na ukatili wa kijinsia katika Jamii.

Related Posts

“juega Gratis A Pine Of Plinko A Couple Of En Modo Demo

Cómo Jugar A Pinus Radiata Of Plinko Two Análisis De Los Angeles Tragaperras” Content Ventajas Y Desventajas Para Pine Of...

Казино Комета официальный Сайт Вход только Регистрация

Комета Казино Oфициальный Сайт Казино Kometa Casino Content как Проходит Процесс Регистрации В Комета Казино? Рабочее Зеркало Kometa Казино —...

Capitolbet Bahis Ve On Line Casino Sitesi

Casino Guess Sitelerinin Adresleri Giriş Adresleri On Line Casino Bet Television Arranged Canlı Maç İzle Content Capitolbet Giriş Lordcasino Giriş...