Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Atembelea Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Kampasi ya Mizengo Pinda

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Techknolojia, Mh. Omary Juma Kipanga akiteta jambo na mwenyeji wake Rasi wa Ndaki ya Mizengo Pinda, Prof Josiah Katani na mkuu wa wilaya ya  Mlele Mh Sanga pindi alipotembelea katika kampasi hiyo.

Wakati huohuo Mh. Kipanga alipata nafasi ya kuzungumza na watumishi wa SUA, Viongozi wa halmashauri ya Mlele pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa ya wilaya.

Mh. Kipanga amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuboresha sekta ya Elimu na katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Sua Kampasi ya Mizengo Pinda imetengewa kiasi cha shilingi Billioni ishirini kwaajili ya ujenzi wa majengo matatu, Jengo la Taaluma, Jengo la Mabweni na Jengo la Daharia.

Pia, Mh. Kipanga amemtaka Rasi wa Ndaki Prof. Josiah Katani kusimamia vyema  fedha inayotolewa na Mh. Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania iendane na thamani ya majengo yatakayojengwa kwa maendeleo ya sekta ya Elimu na Nchi kiujumla.

Related Posts

Mafunzo Elekezi kwa Wafanyakazi wa Kampasi ya Mizengo Pinda kuhusu Ujazaji wa Mfumo wa Taarifa za Utendaji Kazi na Usimamizi wa Wafanyakazi wa Umma (PEPMIS).

Mafunzo ya kipekee yaliyofanyika katika Kampasi ya Mizengo Pinda yameleta mwanga mpya kwa wafanyakazi. Mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Ofisi ya...

Chairperson Professor Josiah Katani Conducts a Special Academic Committee Meeting at Mizengo Pinda Campus.

The Principal, Prof. Josiah Katani plays a pivotal role in overseeing the proceedings and ensuring that the committee’s recommendations align...

Bodi ya Ukaguzi ya SUA Yafanya Ziara katika Kampasi ya Mizengo Pinda

Katika jitihada za kuimarisha ubora wa elimu na utafiti, Bodi ya Ukaguzi ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)...