Prof Raphael Chibunda Awataka Wanafunzi Wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo Kampasi Ya Mizengo Pinda Kutumia Vyema Elimu Wanayoipata Ili Kukabiliana Na Changamoto Ya Ajira

Makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Prof. Raphael Chibunda, amewataka wanafunzi wa Kampasi ya Mizengo Pinda kutumia vyema Elimu wanayoipata ili waweze kukabiliana na changamoto ya ajira kwa kujiunga na kujisajili  katika vikundi ili waweze kupata pesa na kuendesha miradi ya ujasiriamali kama ufugaji wa nyuki, kutoa elimu kwa jamii juu ya ufugaji bora na wenye tija ili kujiongezea kipato na kuachana na dhana ya kusubiria ajira kutoka Serikalini.

Prof. Chibunda ameyasema hayo   tarehe 7 /11/2022, alipotembelea Kampasi ya Mizengo Pinda na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na kujionea maeneo ya mradi wa upanuzi wa kampasi hiyo.

Pia Prof Chibunda ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Mh. Samia Suluhu Hassan, kwa kutenga kiasi cha shilingi Bilioni ishirini kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Kampasi hiyo.

Wakati huo huo Prof. Chibunda alipata nafasi ya kutembelea eneo linalochimbwa kisima cha maji katika Kampasi hiyo na kuendelea kumshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania M.h Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa pesa za maendeleo katika chuo chetu.

Pia, makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo Prof Chibunda akipokea taarifa kutoka kwa katibu wa  kamati ya ufuatiliaji wa ardhi kwa ajili ya upanuzi wa Kampasi ya Mizengo Pinda.

 

Related Posts

Development in Progress: DC Mwanga Inspects Academic and Dormitory Buildings at SUA Mizengo Pinda Campus

The District Commissioner of Mlele, Hon. Alhaj Majid Mwanga, conducted an official visit to the Mizengo Pinda Campus of Sokoine...

Youth Should Embrace Entrepreneurship Opportunities – RC Mrindoko

Katavi Regional Commissioner, Hon. Mwanamvua Mrindoko, has encouraged young people, particularly graduates from higher learning institutions, to take advantage of...

Capacity Building Workshop for Academic Staff and Researchers

As part of ongoing efforts to enhance higher education and research, Prof. Robinson Mdegela and Prof. Gration Rwegasira have conducted...