Rasi Wa Kampasi Ya Mizengo Pinda Prof. Josiah Katani afanya ukaguzi wa maeneo ya shamba la mafunzo lilipo Vilolo ili kuthibiti uingizwaji wa mifugo unaofanywa na wakulima wanaolizunguka eneo hilo

Katika zoezi hilo, Prof. Katani aliambatana na Naibu Rasi wa Ndaki Mipango, Utawala na Fedha Prof. Jeremia Makindara, Bwana Shamba wa Kamapasi ya Mizengo Pinda ndugu Tambalu Alphonsi pamoja na Mhadhiri Msaidizi katika fani ya Misitu ndugu Evaristus Magani.

Ukaguzi huo ulilenga kuangalia namna bora ya uboreshwaji wa uwekaji wa mabango ya makatazo ya uingizwaji wa mifugo katika eneo la Shamba la mafunzo unaofanywa na wakulima wanaolizunguka eneo hilo.

Rasi wa kampasi ya Mizengo Pinda Prof. Josiah Katani akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Usalama Kampasi ya Mizengo Pinda ndugu David Kayombo alipotembelea katika shamba la mafunzo ya chuo hicho lilipo Vilolo Mkoani Katani.

Related Posts

Mafunzo Elekezi kwa Wafanyakazi wa Kampasi ya Mizengo Pinda kuhusu Ujazaji wa Mfumo wa Taarifa za Utendaji Kazi na Usimamizi wa Wafanyakazi wa Umma (PEPMIS).

Mafunzo ya kipekee yaliyofanyika katika Kampasi ya Mizengo Pinda yameleta mwanga mpya kwa wafanyakazi. Mafunzo hayo, yaliyoandaliwa na Ofisi ya...

Chairperson Professor Josiah Katani Conducts a Special Academic Committee Meeting at Mizengo Pinda Campus.

The Principal, Prof. Josiah Katani plays a pivotal role in overseeing the proceedings and ensuring that the committee’s recommendations align...

Bodi ya Ukaguzi ya SUA Yafanya Ziara katika Kampasi ya Mizengo Pinda

Katika jitihada za kuimarisha ubora wa elimu na utafiti, Bodi ya Ukaguzi ya Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)...