Timu Ya Watumishi Wa Kampasi Ya Mizengo Pinda Yatinga Hatua Ya Fainali Ya Michuano Ya VC Cup Inayoratibiwa na Kampasi Ya Mizengo Pinda

Timu ya Watumishi wa Kampasi ya Mizengo Pinda yatinga hatua ya fainali ya michuano ya VC CUP baada ya kuitoa timu ya Watumishi wa Tanesco Kibaoni kwa mikwaju ya penati.

Wakati nusu fainali ya pili ilipigwa kati ya Watumishi Tamisemi Usevya dhidi ya Watumishi wa Muda SUA – MPCC, mchezo uliomalizika kwa mabao 2–1 na kuwawafanya Watumishi wa muda SUA – MPCC kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo.

Hivyo basi mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo utapigwa kati ya Watumishi Tamisemi Kata ya Usevya dhidi ya Watumishi Tanesco Kibaoni, mchezo huo utachezwa October 19 2022, katika Uwanja wa Kampasi ya Mizengo Pinda.

Fainali ya kwanza itachezwa 22 october 2022 kwa upande wa soka la Wanawake kati ya Mateso Queens dhidi ya Manga Queens na fainali ya pili siku hiyohiyo itapigwa kati ya Watumishi SUA – MPCC na Watumishi wa muda SUA – MPCC kwa soka la wanaume.

Mchezo wa mpira wa Pete Timu zilizotinga hatua ya fainali ni Wafanyabiashara Kibaoni watacheza dhidi ya Sharp Rangers ya kata ya Usevya.

Pia kutakuwa na michezo mbalimbali  kama vile, kukimbiza kuku, kukimbia kwenye gunia, mchezo wa Bao, Draft, Karata, kuvuta Kamba, Riadha. n.k

Related Posts

Development in Progress: DC Mwanga Inspects Academic and Dormitory Buildings at SUA Mizengo Pinda Campus

The District Commissioner of Mlele, Hon. Alhaj Majid Mwanga, conducted an official visit to the Mizengo Pinda Campus of Sokoine...

Youth Should Embrace Entrepreneurship Opportunities – RC Mrindoko

Katavi Regional Commissioner, Hon. Mwanamvua Mrindoko, has encouraged young people, particularly graduates from higher learning institutions, to take advantage of...

Capacity Building Workshop for Academic Staff and Researchers

As part of ongoing efforts to enhance higher education and research, Prof. Robinson Mdegela and Prof. Gration Rwegasira have conducted...