Viongozi wa SUA na Wakandarasi wa Ujenzi Wakutana Kujadili Changamoto na Mipango ya Majengo Mapya

Viongozi wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), pamoja na wasimamizi wa majengo kutoka Kampuni ya Crystal Consultants na Kampuni ya Til Contractions, wamekutana na kufanya mkutano katika eneo la mradi wa ujenzi wa majengo mawili yanayojengwa katika Kampasi ya Mizengo Pinda. Majengo hayo ni jengo la taaluma litakalokuwa na madarasa na ofisi, na jengo la bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 600 kwa wakati mmoja.

Mkutano huo ulilenga kujadili maendeleo, changamoto, na mipango inayohusiana na mradi huo. Mbunifu wa majengo kutoka Kampuni ya Crystal Consultants, Linda Kasilima, ameitaka Kampuni ya Til Constractions, ambayo imepata kazi ya ujenzi wa majengo hayo, kuzingatia ubora na viwango vya majengo hayo na kuongeza kasi ya ujenzi ili waweze kumaliza kwa wakati uliopangwa. Aidha, mbunifu wa majengo, Linda Kasilima, amemtaka mkandarasi wa ujenzi huo kuzingatia usalama wa wafanyakazi kipindi chote cha ujenzi.

Wakati huohuo, Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Maendeleo cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Ibrahim Mjema, ameipongeza Kampuni ya Ujenzi ya Til Constractions kwa kasi wanayoionyesha katika ujenzi huo. Pia, amewataka kuendelea na kasi hiyo yenye viwango na ubora ili kumaliza ujenzi huo kwa wakati uliopangwa.
Katika mkutano huo, viongozi walipata nafasi ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi kupitia kazi ambazo zimeanza kufanyika. Waliona hatua mbalimbali zilizochukuliwa katika ujenzi wa majengo hayo na waliridhishwa na juhudi zinazofanywa kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati uliopangwa na kwa viwango vinavyohitajika.

Related Posts

“juega Gratis A Pine Of Plinko A Couple Of En Modo Demo

Cómo Jugar A Pinus Radiata Of Plinko Two Análisis De Los Angeles Tragaperras” Content Ventajas Y Desventajas Para Pine Of...

تجربتي مع استخدام هكر 1xbet مجانا

فهم هكر 1xbet مجانا: دليل شامل Content هكر لعبة Accident 1xbet مجانا ازاي تكسب 1500$ يوميا Formula Behavior 1xbet معلومة...

Juego Plinko Es Real O Estafa? Plinko Ha Sido Seguro? Plinko Casino

Plinko: ¿esta Aplicación Es Confiable To Una Estafa?” Content Estrategias De Entrenamiento Plinko: Como Esconden Mis Juegos Adonde Supuestamente Puedes...